.

9/09/2021

Rais Aielezea Royal Tour, Mfahamu Mtangazaji wakeRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ameeleza kuwa Royal Tour ni kipindi maarufu duniani kitakachotumika kurusha makala maalum anayoiandaa itakayoonesha vivutio vya utalii vilivyopo nchini.

Rais Samia ameyabainisha hayo leo Septemba 9, 2021, kupitia ukurasa wake wa Twitter.

"Nimeshiriki kuandaa makala ya Tanzania itakayorushwa katika kipindi maarufu duniani cha Royal Tour, ni matarajio yangu kuwa makala hii itasaidia kuitangaza vizuri nchi yetu, kuinua utalii, kuvutia wafanyabiashara na wawekezaji na kuondoa upotoshaji wa makusudi kuhusu Tanzania," ameandika Rais Samia.

The Royal Tour ni kipindi maalum kinachotoa nafasi kwa viongozi wenye ushawishi kuonesha vivutio, utamaduni na maeneo ya kitalii ya nchi husika yanayomfanya mtazamaji wa kipindi hicho kuvutiwa na kutamani kwenda kuyatembelea, mtangazaji na mzalishaji wa kipindi hicho anaitwa Peter Greenberg.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger