Rais Kagame awaonya Warwanda dhidi ya kuingia Uganda, adai watateswa

Rais Kagame alishtumu Uganda kwa kuwakamata na kuwatesa raia wake
Kigame alisema iwapo Warwanda watavuka mpaka na kuingia Uganda, watakamatwa na kupigwa
Rwanda iliweka marufuku ya kuingia Uganda mnamo Machi 2019 na kufunga mpaka wake na Uganda
Rais wa Rwanda Paul Kagame amefichua uhasama kati ya taifa lake na nchi jirani ya Uganda baada ya kuwaonya raia wake kuzuru nchi hiyo.

Rais Kagame Awaonya Warwanda Dhidi ya Kuenda Uganda "Mutateswa"
Rais Paul Kagame katika mkutano wa awali.Picha:Paul Kagame.
Katika mahojiano na shirika la habari la serikali, Rwanda Broadcasting Agency, Jumapili, Septemba 5, Rais Kagame alishtumu Uganda kwa kuwakamata na kuwatesa raia wake.

“Kuna tu njia moja pekee kuzuia hii shida kwa kutoenda huko (Uganda). Usiende huko kwa sababu ukivuka mpaka na wakukamate, wakuchape ama wakuibie, na urudi, unataka nifanye nini."

“Hiyo ni nchi nyingine inayolindwa na sina mamlaka katika nchi hiyo. Ushauri pekee naweza kupa ni usiende Uganda,” Kagame alisema.


 
Rwanda iliweka marufuku ya kuingia Uganda mnamo Machi 2019 na kufunga mpaka wake na Uganda.

Haya yalikujia baada ya Rwanda kukashifu Uganda kuwahifadhi na kuwafadhili waasi.

Kwa upande mwingine Uganda imeshtumu Rwanda kwa kuwatuma wajasusi kufanya upelelezi nchini humo.


Mikutano kadhaa ya faragha iliyowahusisha viongozi wa mataifa ya ukanda huo yakiwemo Angola na DRC haijazaa matunda katika kusuluhisha mgogoro kati ya mataifa hayo mawili.

Mnamo Agosti 2019, marais Kagame na Museveni walikutana katika mpaka wa Gatuna na kutia saini kile kilionekana kama mkataba wa makubaliano ya kuhimarisha uhusiano wao.

Wawili hao walikubaliana kujiepusha na hatua ambazo zitazua mpasuko kati yao.

Kamati ya Adhoc ikiongozwa an mawaziri wa masuala nje ilikuwa imepiga hatua katika kuanza kutekeleza makubaliano hayo baada ya misururu ya mikutano mijini Kigali na Kampala.


 
Mchakato huo ulisitishwa kufuatia chimbuko la janga la COVID-19 ambalo lilizuia usafiri na tofauti kuibuka kuhusu namna makubaliano hayo yalitekelezwa.

Kutokana na hali ya COVID-19 nchini Uganda, shirika la ndege la Rwanda pia lilisitisha safari za Entebbe mnamo Juni na hivyo kuwa vigumu kwa Warwanda kusafiri Uganda.

Mamlaka nchini Uganda ilikuwa imelalamika kuwa Rwanda inazuia kusafirishwa kwa mizigo yake kupitia Burundi na Tanzania.

Mapema Mei, iliibuka kuwa Uganda na Burundi zilikuwa zinamalizia mipango ya kujenga barabara mpya kuhimarisha biashara yao kwa sababu ya Rwanda kufunga mpaka wake na Uganda.


Barabara hiyo inatazamiwa kupitia kaskazini mwa Tanzania na kuunganishwa na mpaka wa Burundi wa Kobero.

đŸ’¥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SERIKALINI

đŸ’¥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SEKTA BINAFSI

đŸ’¥NAFASI ZA INTERSHIP MAKAMPUNI MBALI MBALI

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad