Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Rais Samia Anatarajia Kuondoka Nchini Kesho Kuelekea New York Nchini Marekani

 


Rais Samia anatarajia kuondoka nchini leo kuelekea New York nchini Marekani kuhudhuria Mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ambapo tarehe 23 anatarajiwa kulihutubia Baraza hilo.

Pamoja na Mkutano huo Rais Samia atahudhuria mikutano ya kilele ya kujadili masuala ya mabadiliko ya tabia nchi, usalama wa chakula na utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) .

Rais Samia anatarajiwa pia kukutana na Wakuu wa Nchi nyingine na Viongozi wa Mashirika ya Kimataifa kwa lengo la kuimarisha ushirikiano na uhusiano baina ya Tanzania na Nchi na Taasisi zao.

 HABARI KAMA HIZI DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL KWA KUBONYEZA > HAPA

Post a Comment

0 Comments