Rais Samia: Sitaki Kuwaona Kwenye TV tu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA
Rais Samia Suluhu amewataka Viongozi wateule walio apishwa leo Septemba 13, 2021 kuhakiksha kuwa wanakwenda kufanya kazi kwa bidii ikiwa ni pamoja na kutimiza majukumu yao kwa weledi na kwa wakati maalumu.

 

Amesisitiza kuwa anachotaka kukiona ni matokeo chanya katika nafasi hizo walizopangiwa na sio viongozi hao kuonekana kwenye televisheni pekee.

 

“Nachotaka kuona ni matokeo ‘Results’ sitaki kuwaona kwenye Tv tu nataka Results kwa wananchi, mkaanze kwa kasi pale wenzenu walipoachia, nataka muende kwa haraka muda hautusubiri nataka nione Results, naposema nataka nione Results sio kwa wapya tu hata nyie wa zamani nataka mjipange upya.

 

“uteuzi wenu haina maana nyie ni wazuri kuliko wengine hapana, uzuri wenu utaonekana katika utekelezaji wa majukumu yenu kwa sababu hata tulio wachagua mwanzo walikuwa wazuri pia,” amesema Rais Samia.

 

Aidha ametolea ufafanuzi suala la uteuzi wa Waziri wa Ulinzi kuwa wa jinsia ya kike, kuwa amefanya maamuzi ya kuteuwa hivyo ili kubadilisha utamaduni ulio jengeka miaka mingi kuwa nafasi hiyo ni ya jinsia ya kiume.

 

“Nimeamua kuvunja taboo ya muda mrefu kwamba Wizara ya Ulinzi lazima akae Mwanaume mwenye misuli yake lakini kazi ya Waziri kwenye Wizara ile sio kupiga mizinga wala kubeba bunduki ni kusimamia sera na utawala wa Wizara, nikaamua Dada yetu Dr. Tax nimpeleke huko,” amesema Rais Samia.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad