.

9/15/2021

Rais Samia: Ukivunja Sheria UtashughulikiwaRAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema kuwa iwapo akitokea mtu yeyote kutaka kuvunja sheria za nchi atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

 

Rais Samia amesema hayo leo Jumatano, Septemba 15, 2021 wakati akizungumza kwenye kongamano la Siku ya Demokrasia duniani.

 

“Haki za binadamu nazo zimetambuliwa katika katiba yetu na nchi yetu imesaini na kuridhia mikataba ya kikanda na kimataifa kuhusu haki za binadamu.

 

“Nchi yetu inaongozwa kwa mujibu wa sheria ambapo hakuna mtu aliye juu ya sheria, ukivunja sheria basi utashughulikiwa na haichagui yoyote yule.

 

“Nchi yetu ina vyama vya siasa takribani 20, tuna vyama vya wafanyakazi, wanataaluma mbalimbali na uhuru wa kukusanyika upo kwa kiasi kikubwa na hii ndio sababu tumeweza kukusanyika hapa kuadhimisha siku ya Demokrasia,” amesema Rais Samia.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger