Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Saddam Hussein: Siri ya Toleo la Qur'an lililoandikwa kwa 'Lita 24 za Damu' ya Rais wa zamani wa Iraq

Mwishoni mwa miaka ya 1990, Saddam Hussein alimwendea mpiga picha akiwa na ombi la kushangaza.

Saddam Hussein, ambaye aliingia madarakani mnamo mwaka 1979, alibakia kuwa rais wa Iraq hadi uvamizi ulioongozwa na Marekani mnamo 2003. Alitaka kutengeneza nakala ya Kitabu kitakatifu cha Qur'an kwa kutumia damu yake badala ya wino.

Kulingana na hadithi hiyo, Saddam Hussein alikuwa akitoa mkono wake kwa muuguzi kila wiki kwa miaka miwili ili aweze kuchota damu yake ambayo angetumia kuandika Qur'an.

Pamoja na gharama zinazohusika, maelezo mengine mengi ni ya kutatanisha. Lakini kulingana na madai ya mara kwa mara, Saddam Hussein alitumia lita 24 za damu kuandika kurasa 605 (114 suras) za Qur'an.

Joseph Sasson, mkurugenzi wa Kituo cha Mafunzo ya Kiarabu ya Kisasa katika Chuo Kikuu cha Georgetown nchini Marekani, anasema Qur'an iliwasilishwa kwa Saddam Hussein kwa shangwe kubwa. Sasson pia ni mwandishi wa kitabu kuhusu Saddam Hussein.

"Saddam alijivunia sana," alisema Samuel Halfont, Profesa wa mkakati wa kisiasa katika Shule ya Uhitimu ya Naval huko California. Alitengeneza picha nyingi na hii Qur'an.

Nakala tofauti ya Qur'an ilihifadhiwa katika Msikiti wa Umm al-Qura huko Baghdad. Msikiti huu pia ulijengwa na Saddam Hussein na una minara minne mikubwa. Wengine wanaamini mnara huo unafanana na ncha ya Kalashnikov (AK-47).

Hafla ya uzinduzi wa Qur'an ilifunikwa na vyombo vya habari vya Iraq na kimataifa. Kulingana na ripoti kutoka Septemba 25, mwaka 2000, Saddam Hussein aliunda toleo hili la Qur'an ili kumlinda na "njama na hatari" katika safari yake ya kisiasa.

Msikiti wa Umm al-Qura huko Baghdad ulijengwa na Saddam Hussein na ndipo nakala hii ya Qur'an ilihifadhiwa.


Katika barua iliyotolewa kwa vyombo vya habari vya serikali wakati huo, Saddam Hussein alisema: "Maisha yangu yako hatarini na ningeweza kupoteza damu nyingi. Lakini nilipoteza damu kidogo. Kisha nikauliza kwamba maneno ya Kitabu cha Mungu yaandikwe kwa damu yangu kama dhabihu.

Watu wengine wanafikiri kwamba walifanya hivyo kwa sababu walikuwa wakipitia shida inayokabili matabaka yao wakati huo. Wataalamu wengine wanaamini alitaka kufanya hivyo kwa sababu alikuwa akimshukuru Mungu kwamba mtoto wake, Adi Saddam Hussein, alikuwa amenusurika na shambulio la Septemba mwaka 1996.

Lakini kulingana na Sasson, sababu ilikuwa nyingine.

'Matumizi ya dini kwa madhumuni ya kisiasa'
Sasson anasema Qur'an iliyojaa damu ni mfano wa jinsi dikteta anaweza kutumia chochote kufikia malengo yake ya kisiasa, bila kujali dini.

Jinsi Bin Laden, Saddam na Gaddafi walivyosakwa na kukamatwa au kuuawa
"Mwisho wa vita na Iran mnamo miaka ya 1990, Saddam aligundua kuwa mawazo ya kidini ya Iran yanaegemea Iraq." Alisema wazi kuwa vijana wa chama cha Ba'ath walikuwa wakiugeukia msimamo mkali.

"Sidhani kama walikua waumini zaidi," Sasson alisema. Walianza onesho hili kwa madhumuni ya kisiasa.

Picha iliyopigwa mwezi Novemba mwaka 1988, ikimuonesha Saddam Hussein na familia yake


Anasema alijenga misikiti na chuo kikuu kikubwa, ambacho alikiita taasisi kuu ya masomo ya Qur'an. Alifikiri ni wazo zuri kwa sababu alifikiri ingewashawishi watu kuunga mkono chama chake. Watasoma Qur'an kwa njia ambayo wataichukulia kama mwongozo wao. Hii itawarahisishia kudhibiti watu kupitia dini.

Anatoa mfano wa Saddam Hussein, ambaye alibadilisha mtazamo wake kwa wanawake ili kufikia malengo yake. "Alipoingia kwenye siasa mnamo 1968, alikuwa akicheka mila. Alitaka wanawake wawe na haki ya kupiga kura, wafanyikazi wawe na haki na fursa za elimu kwa wote.

"Alikuwa mtetezi wa kweli wa jukumu la wanawake katika jamii lakini mnamo mwaka 1990 alibadilisha sauti yake na kuanza kusema kuwa wanawake wana nafasi nyumbani na kazi yao ni kupata watoto wengi iwezekanavyo."

Anasema kulikuwa na sababu mbili. "Ushabiki wa kidini na ukosefu wa ajira viliongezeka. Wanajeshi milioni saba waliuawa katika vita na Kuwait.

Kulingana na Sassoon, alitaka kazi za wanawake ziende kwa wanaume (kama ilivyotokea Ulaya baada ya Vita vya Kwanza vya dunia) ili kupunguza mivutano ya kijamii inayosababishwa na ukosefu wa ajira.

Lita 24 za damu zadaiwa kutumika kuandikia Qur'an
Halfont ameiambia BBC kuwa lita zenye damu zikiwa zimeongezewa na kemikali tofauti zitatumika kama wino.

Je, inaweza kuwa damu ya Saddam Hussein?
Kwa mujibu wa Sassoon,ni kweli Saddam alimpatia damu yake, lakini bado ana wasiwasi damu yote sio ya kwake, kwasababu ni ilihitajika nyingi zaidi kwenye karatasi zote.Inakadiriwa mtu anaweza akachangia hadi 470 ml za damu kwa vipindi vinne ndani ya mwaka.

Hii inaonesha ni dhahiri Saddam alichangia yote hii kwa vipindi kwa miaka mitatu.Wataalamu wanasema alikuwa anaogopa, ukilinganisha na utamaduni wa taifa hilo wa kupeana mkono, kwa Saddam lilikuwa jambo la tofauti hakupenda kufanya hivyo kwa wageni waliofika kwenye Ikulu yake.

"Alikuwa akihofia kupata mafua," anasema Sasson. Wakiwa mezani hawakuweza kula wala kunywa chochote. Alikuwa na mpishi wake anayemhudumia yeye lakini bado mahabara ilikuta akiwa amewekewa sumu kwenye chakula.

."Kwahiyo siwezi kuwa ni kweli ama sio kweli, lakini kutokana na yaliokuwa yamemtokea aliamua kuchangia damu ili itumike kuandikia Qur'an."

Ifutwe au ifichwe?


Anguko la serikali ya Saddam Hussein mwaka 2003,toleo la Qur'an lilioandikwa kwa damu ulifichwa.

Alifungiwa na kutoruhusiwa kutoka kwenye msikiti.

Ilihitajika funguo tatu kufikia chumba kilichofichwa Qur'an hatahivyo sio karatasi zote zilikuwemo.

Mwandishi wa habari alinyimwa nakala za karatasi hizo nakuambiwa kuwa ni ili aipate itabidi apate idhini ya kamati.

Abbas Shakir Judi, ambaye alihusika kuandika chapisho lake aliamua kuihama Iraq na kuishi Marekani jimbo la Virginia.

Massanamu mengi ya Saddam Hussein yaliondolewa Iraq mwaka 2003. Majengo yaliyokuwa yanaumiliki wake yalibinafsishwa lakini bado watawala walibaki njia panda uwapi msaaafu.

Kwa mujibu wa Halfont, jambo hili limeonekana kuwa ni suala la kiimani zaidi.

"Kwa upande mwingine wa viongozi na wanazuoni wa dini wanasema kuwa damu iliyotumika haikuwa safi kutokana na matendo ya mhusika wa damu hiyo, vilevile hakuna historia kwenye Uislamu inayoelezea kuwa msaafu iliandikwa kwa damu."

Ameongeza kuwa jambo la kutoitafuta halitosaidia , baadhi ya watu waliokuwa na vipande vya nakala wanaeleza kuwa bado zipo.

Wengine wanasema lilifanyika jambo la siri la kuipatia Saudi Arabia kama zawadi, huku wengine wakiamini kuwa kwa sasa msaafu huo unamilikiwa na mtoto wa Saddam Hussein anayeishi Jordan, ila hakuna wa kuthibitisha hilo.

Muandishi kutoka Ufaransa Emmanuel Carey akishirikiana na Lucas Mangat waliamua kusafiri mpaka Baghdad mwaka 2018 huku lengo kuu likiwa ni kutafuta Msaafu huo, lakini mpaka wanaondoka hawakuweza fanikiwa kuupata.

Je iko wapi Qur'an hiyo?


Maelezo ya picha, Saddam Hussein
Unaweza kukuta msaafu huo umefichwa kwenye msikiti mmoja wapo huko Baghdad.

Marekani ilipoingia nchini humo, mtu aliyehusika na karatasi hizo aliliambia gazeti la Uingereza The Guardian kuwa "zinahitajika funguo tatu kupata karatasi nyingime…."

Huku mmoja akiwa anao yeye, mwingine mkuu wa polisi na wa tatu ukiwa Baghdad

 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments