.

9/10/2021

Safari za ndege zaanza tena Kabul Afghanistan
Safari za ndege za kimataifa zimeanza tena nchini Afghanistan, ikiwa hatua muhimu kwenye juhudi za serikali mpya ya Taliban kurejesha hali ya kawaida baada ya kutwaa madaraka mwezi uliopita.
Ndege ya shirika la ndege la Qatar iliondoka jana kuelekea Doha ikiwa na abiria 113, wakiwemo raia wa Ujerumani, Marekani, Canada na Uingereza. Msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni ya Marekani, Ned Price, amethibitisha kuwa raia 10 na wakaazi 11 wa kudumu wa nchi hiyo walikuwemo kwenye ndege hiyo. 
 
Mjumbe maalum wa Qatar nchini Afghanistan, Mutlaq bin Majed al-Qahtani, amesema safari hii ni ya kawaida na si sehemu ya kampeni ya kuwahamisha watu wanaotaka kuikimbia Afghanistan. 
 
Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Qatar, Sheikh Mohammed bin Abdulrahman Al-Thani amewashukuru viongozi wa Taliban kwa kusaidia kwenye kuufunguwa tena uwanja mkubwa wa ndege wa Kabul.
 
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger