.

9/03/2021

Salama Jabir Aacha Kazi EATV, Ahusishwa Kujiunga na Simba Kama MsemajiMtangazaji nguli nchini na kipenzi cha wengi, Salama Jabir jana alitangaza kuachana na kituo cha EATV ambacho amefanya kazi hapo kwa muda wa takribani miaka 19 huku sababu kuu ikiwa ni kwenda nje ya media hiyo kuona pia hali ikoje.

Salama amekuwa EATV kwa muda mrefu akijizolea umaarufu zaidi na vipindi kama Mkasi ✂, Shabiki On Saturday (SOS) pamoja na kipindi cha SALAMA NA..

Lakini tetesi zimekuwa nyingi mitandaoni kuwa uwenda akawa msemaji wa klabu ya Simba SC japo mwenyewe amekataa kuwa si kweli na yeye anaziona habari hizi kwenye mitandao ya kijamii kama tunavyoona sisi.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger