Senzo: Tunaenda Kuijenga Yanga Mpya

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA





OFISA Mtendaji Mkuu wa Yanga (CEO), Senzo Mazingisa, amesema wamejiandaa kufanya kazi bora na kuijenga Yanga mpya na imara kwa ajili ya kuongeza chachu ya mafanikio zaidi ili kutimiza malengo yao, ikiwemo kutwaa mataji mbalimbali.


Senzo hivi karibuni aliteuliwa na uongozi wa timu hiyo kuwa CEO katika klabu hiyo akitoka katika cheo cha mshauri mkuu wa masuala ya mabadiliko ya klabu hiyo.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Senzo alisema kuwa wao kama viongozi wamejipanga kufanya kazi kubwa ndani ya Yanga kwa ushirikiano ili kufikia malengo ya timu.

 

“Sisi kama viongozi tumejiwekea malengo yetu ambayo mojawapo ni kuifanya Yanga ifikie katika hatua kubwa ya mafanikio kwa kufanya kazi kwa ushirikiano ili tufikie hayo malengo.


“Tumejipanga vema kabisa kuhakikisha tunaifanya kazi hii kwa uzuri kabisa na niseme tu kuwa sasa tunaenda kufanya kazi ya kuifikisha katika kilele cha mafanikio ikiwa ni pamoja na kubeba mataji ya michuano mbalimbali,” alisema kiongozi huyo.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad