Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Simanzi Maiti ya Mchezaji Ghana “Kudhalilishwa”
Maiti ya aliyekuwa mshambuliaji wa Blackstars na Kumasi Asante Kotoko, Godfred Yeboah imewatia wengi simanzi. Mchezaji huyo raia wa Ghana ambaye ni maarufu kwa jina la Tv3, alifariki Agosti 3 mwaka huu katika hospitali ya Mkoa wa Sunyani baada ya kuugua kwa muda mfupi.

 Hata hivyo, jambo ambalo limezua gumzo mitandaoni ni namna mchezaji huyo alivyozika ambapo inaelezwa kuwa maiti yake ilivalishwa jezi na kusimamishwa na  kushikishwa mpira kisha baadaye kuzikwa.Kitendo hicho siyo tu kiliwahuzunisha waombolezaji waliojitokeza kwenye mazik ya mchezaji huyo lakini kimegusa mioyo ya wengi  hasa baada ya picha za maiti hiyo kusambazwa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii.Wengi waliozitazama wamekemea kitendo hicho na kusema kilijaa udhalilishaji wa maiti ya mchezaji huyo ambaye mazishi yake yalihuzuliwa na wachezaji wenzake nguli.

@manyota_rich

 HABARI KAMA HIZI DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL KWA KUBONYEZA > HAPA

Post a Comment

0 Comments