Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

SIMBA Wanahitaji Kikao Cha Dharura Msimu HuuNA @johnharamba

Nauona mtihani mgumu kwa Simba msimu huu, hilo litakuwa na uhalisia kama hawatachukua hatua za haraka na za dharura katika mambo kadhaa.

MORALI YA WACHEZAJI
Kibinaadamu ukishapata vitu vingi au kila unachoshindania ni jambo la kawaida morali kushuka, sababu unakuwa huna hasira za ukweli za kupambania kitu au vitu ambavyo unavyo.

Simba wametawala soka la Tanzania kwa msimu minne mfululizo, wameshinda mataji yote ya ndani kwa kipindi hicho, kwa nje wamepata mafanikio mazuri japo hawajabeba taji. Hapo ni wazi kunahitajika kitu cha ziada kubadili akili za wachezaji wanapovaa jezi ya Simba.

YANGA WANAAMKA
Yanga ndiyo wapinzani wakubwa wa Simba, baada ya kuonewa kwa miaka kadhaa, ni kama wanaelekea kuamka, hawajafikia katika ubora mzuri lakini taswira inaonyesha kuwa wana jambo lao.

Hivyo, Simba kama hawatashtuka mapema kuna uwezekano wa kupata tabu kutoka kwa Yanga kama wataendelea kuwa ‘serious’.

WAPINZANI WAMEJIPANGA
Siyo kwamba miaka hii minne walikuwa hawajajipanga lakini safari hii watazame Yanga, Azam FC, Mtibwa Sugar, ni aina ya timu ambazo lazima zimepania kufanya kitu kwa aina ya usajili na jinsi walivyoboresha mabenchi ya ufundi.

USAJILI MPYA UNAHITAJI MUDA
Wapo wachezaji ambao wakisajiliwa paap nao wanaonyesha uwezo wao, wengine wanahitaji muda, Simba ina wachezaji wengi wapya na inavyoonekana wanatakiwa kuingia kikosi cha kwanza, dalili zinaonyesha bado hawajawa na chemistry nzuri na wenzao.

BWALYA VIATU VYA CHAMA VIKUBWA
Wakati anasajiliwa alichukuliwa poa kwa kuwa kulikuwa na mfalme Chama, baadaye alivyozoea mazingira akaanza kuuwasha moto, lakini nimeshuhudia mara kadhaa Bwalya akishindwa kuibeba timu pindi inapokuwa imepoteana.

Licha ya kuwa Chama kuna baadhi ya mechi za Yanga alikuwa hapafom vizuri lakini mechi nyingi kubwa alionyesha nini maana ya kui-control timu kwa miguu yake. Kwa sasa hayupo, mzigo huo upo kwa Bwalya, nina hofu kama ataweza kuibeba Simba mgongoni katika mechi nyingi mfululizo.

 Downlaod App ya BLOG Hii Kutoka Google Play Kwa Kubonyeza HAPA>>>

Post a Comment

0 Comments