Ticker

6/recent/ticker-posts

Taifa Stars Yaitungua Madagascar 3-2TIMU ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imefanikiwa kuondoka na pointi tatu mbele ya Timu ya Taifa ya Madagascar katika mechi yake ya mzunguko wa pili ya kuwania kufuzu mashindano ya Fainali za Kombe la Dunia.

 

Stars imeibuka na ushindi wa bao 3-2 dhidi ya Madagascar katika Dimba la Mkapa jijini Dar es Salaam, leo Jumanne, Septemba 7, 2021.Mabao ya Stars yamefungwa na;

⚽️Erasto Nyoni 2′
⚽️Novatus Disma 26′
⚽️Feisal Salum 52′

 

Mabao ya Madagascar yamefungwa na;

⚽️Njiva Rakotoharimalala 32′
⚽️Thomas Fontaine 45+2′.

 

Stars sasa inaongoza Kundi J la michuano hiyo ikiwa na pointi nne sawa na Benin ambao pia wana pointi nne. Nafasi ya tatu ni DR Congo mwenye pointi 2 na anayeburuza mkia ni Madagascar ambaye hana pointi hata moja katika michezo yote miwili aliyocheza.

 

Stars inajiweka kwenye nafasi nzuri ya kusonga mbele katika mashindano haya iwapo itahakikisha mechi zote za nyumbani zilizosalia inashinda ikiwa ni mechi dhidi ya Congo (ya marudiano) na ile ya Benin.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments