Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Ulaya yasema Iran iko tayari kurejea kwenye mazungumzo ya nyuklia

Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya, Josep Borell amesema mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa Iran amemuhakikishia kwamba nchi hiyo iko tayari kuanza tena mazungumzo kuhusu makubaliano ya nyuklia hivi karibuni. 
Taarifa ya Umoja wa Ulaya imesema leo kuwa Borrell alisisitiza kwa mara nyingine tena umuhimu mkubwa wa kuanza mazungumzo ya Vienna katika mkutano uliofanyika jana kati yake na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Hossein Amir-Abdollahin pembezoni mwa mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. 

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Amir-Abdollahin amehakikisha utayari wa kuanza tena mapema kwa mazungumzo. 

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Saeed Khatibzadeh amesema anatarajia mazungumzo hayo yataanza tena katika wiki zijazo, bila ya kutaja tarehe kamili.

 HABARI KAMA HIZI DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL KWA KUBONYEZA > HAPA

Post a Comment

0 Comments