Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Wafunga Ndoa Wodini Baada ya Bwana Harusi Kupata Ajali ya Boda


Augustine Makule na Mpenzi wake Rose Kimaro wamefunga ndoa wodini jijini Dodoma baada ya Bwana harusi kupata ajali ya Bodaboda siku mbili kabla ya siku ya harusi yao.

Ajali hiyo ya pikipiki iliyotokea eneo la zuzu Dodoma na kupelekea kijana Agustino kukatwa mguu wake wa kulia na vidole vitatu vya mguu wake wa kushoto.

Licha ya maumivu makali aliyokuwa nayo waliamua kuendelea na ratiba yao ya ndoa ambayo waliifungia ndani ya wodi baada ya Mchungaji kufika na baadhi ya Waumini na kuendelea na taratibu za ndoa, full video ya habari hii ipo kwenye Youtube ya millardayo.

 Downlaod App ya BLOG Hii Kutoka Google Play Kwa Kubonyeza HAPA>>>

Post a Comment

0 Comments