.

9/11/2021

Wafungwa wanne kati ya sita waliotoroka gerezani wakamatwa tena

Wafungwa wanne kati ya sita wa Kipalestina waliotoroka kutoka jela yenye ulinzi mkali mapema wiki hii wamekamatwa, polisi wa Israeli wanasema.

Wawili walipatikana katika maegesho ya magari mapema asubuhi ya Jumamosi, polisi walisema.

Wengine wawili walikamatwa karibu na jiji la Nazareti Ijumaa.

Msako ulianzishwa Jumatatu baada ya wafungwa hao sita kutoka nje ya gereza la Gilboa kaskazini mwa Israel, tukio la kwanza la kutoroka gereza la Palestina kwa kiwango hiki kwa miaka 20.

Makundi ya wapiganaji wa Palestina wakati huohuo yalisifu kutoroka kwao wakikiita kitendo hicho kuwa cha "kishujaa".

Wafungwa hao waliotoroka wanaaminika kuchimba shimo kwenye sakafu ya gereza lao kwa miezi kadhaa na kuweka shimo kuelekea chini ya gereza.

Wanafikiriwa kutambaa kupitia shimo hilo na kufikia ukuta wa nje wa gereza, kisha wakachimba handaki lililoibuka katikati ya barabara ya udongo, chini tu ya mnara wa walinda usalama.

Picha za CCTV ziliwanasa wakiacha handaki saa 01:30 Jumatatu. Lakini kengele ilipigwa saa 04:00 alfajiri baada ya wenyeji kuripoti kuona "watu wanaoshukiwa kuwa wafungwa" katika uwanja karibu na gereza.

Vyombo vya habari vya Israeli vimeshutumu kutoroka jela kwa wafungwa hao vikiashiria kuzorota kwa usalama.

Walijumuisha uchapishaji wa mwongozo wa gereza kwenye wavuti ya wasanifu waliohusika katika ujenzi wake; kuwekwa kwa wafungwa sita kutoka mji wa Jenin Ukingo wa Magharibi katika chumba kimoja, wakiwemo watatu wanaochukuliwa kama hatari kubwa ya kutoroka; na uamuzi wa kutowasha kifaa cha ambacho kingewazuia kutumia simu za mkononi zilizoingizwa kwa siri ili kuwasiliana na watu nje ya gereza.

Kulikuwa pia na ripoti ambazo hazijathibitishwa kuwa mlinzi huyo alikuwa amesimama kwenye mnara karibu na njia ya handaki alikuwa amelala wakati walipokuwa wakitoroka.

Mmoja wa waliokamatwa ni Zakaria Zubeidi, ni kamanda wa zamani wa Brigedi ya Al-Aqsa huko Jenin. Alikamatwa na vikosi vya Israel mnamo 2019 kwa tuhuma za kuhusika katika mashambulio kadhaa ya risasi.

Wengine watano - Mahmoud Ardah, Mohammed Ardah, Iham Kamamji, Yaqoub Qadri na Munadil Infaat - ni wafuasi wa kundi la wapiganaji la Islamic Jihad. Wanne kati yao wanatumikia vifungo vya maisha baada ya kutiwa hatiani kwa kupanga au kutekeleza mashambulio yaliyowaua Waisraeli.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger