.

9/02/2021

Wanafunzi wengine 73 watekwa Nigeria
Wanafunzi 73 wametekwa nyara na watu wenye silaha katika shule ya sekondari ya kaskazini magharibi mwa Nigeria.
 
 Kulingana na taarifa rasmi ya polisi, Kundi la watu wenye silaha lilivamia shule hiyo ya eneo la Kaya katika mkoa wa Maradun la Jimbo la Zamfara mapema jana asubuhi, na kuwateka nyara wanafunzi hao. 
 
Timu za uokozi za polisi zinafanya kazi pamoja na wanajeshi kujaribu kuwakomboa wanafunzi hao, amesema msemaji wa polisi Mohammed Shehu. Utekaji nyara wa wanafunzi umekuwa ni jambo lilozoeleka kaskazini magharibi na katikati mwa Nigeria. 
 
Karibu wanafunzi 1,000 walitekwa mwaka huu - na baadae wengi wao waliachiliwa. Rais Muhammadu Buhari yuko chini ya shinikizo kutokana na nchi yake kukosa usalama. 
 
Licha ya juhudi za wanjeshi za kupambana na wahalifu hao, mashambulizi na utekaji nyara bado yanaendelea.
 
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger