Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Wanahabari Wapata Ajali Geita
Waandishi wa habari mkoani Geita, Consolata Evarist wa Global TV, Esther Sumira wa Azam TV na Muta Robert wa Majira, wamenusurika kifo katika ajali baada ya gari aina ya Pajero Mitsubish waliyokuwa wanatumia kuacha njia na kuanguka.

 

Consolata na wenzake walikuwa wanaelekea Wilaya ya Nyang’hwale mkoani Geita kutafuta habari ambapo walipata ajali hiyo wakiwa hawajafika safari yao.

 

Akizungumza na Global TV Online, Consolata alisema, wanamshukuru Mungu kwani licha ya gari walioyokuwa wakitumia kuanguka lakini wao wametoka salama zaidi wamepata maumivu madogo madogo.

 

Alisema baada ya kutoka salama, taratibu za kipolisi zimefanyika na wao kuweza kuendelea na majukumu yao ya kazi.


 HABARI KAMA HIZI DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL KWA KUBONYEZA > HAPA

Post a Comment

0 Comments