Wanaume wenye umri mkubwa waonywa kuwa na mahusiano wasichana wadogo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Dodoma. Serikali ya Tanzania imewaonya wanaume wenye umri mkubwa kuachana na tabia ya kujihusisha na mapenzi na wasichana wadogo.
Kauli hiyo imetolewa leo Alhamisi Septemba 8,  2021 na naibu Waziri wa Nchi  Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia wenye ulemavu,  Ummy Ndeliananga wakati akifungua mkutano wa vijana wanaoishi na virusi vya ukimwi.

Amesema vijana wadogo wa kike kuwa na mahusiano ya kingono na wanaume wenye umri mkubwa kwa kuvutika na vishawishi kama  pesa na zawadi ndogo ndogo.

“Kwa mara nyingine tena natoa rai kwa wanaume wenye umri mkubwa kuachana na tabia ya kujihusisha na mapenzi na wasichana wadogo,”amesema.

Amesema Serikali haitasita kuchukua hatua kali za kisheria kwa yeyote atakayebainika kujihusisha na vitendo hivyo.

Aidha, Ummy amesema takwimu zinaonesha kuwa vijana wengi wanaojihusisha na mapenzi hawatumii kinga na wengine hutumia mara moja tu na baada ya kuzoeana huendelea na mahusiano ya ngono bila kinga yoyote.

Mwenyekiti wa Baraza la Watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (Nacopha),   Leticia Kapela amesema pamoja na jitihada hizo, bado kuna changamato zinazoendelea kujitokeza siku hadi siku.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad