.

9/06/2021

Wanne Wafariki kwa Ajali Kagera

WATU wanne ambao majina yao hayakupatikana haraka wamefariki dunia na wengine 33 kujeruhiwa baada ya basi la kampuni ya Fikosh lenye namba za usajili T 710 BXB kuacha njia na kupinduka katika mteremko wa Nyangoye ulioko katika manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.Kamanda wa polisi mkoani Kagera Revocatus Malimi amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo na kwamba miongoni mwa waliopoteza maisha watatu ni watu wazima na mmoja ni mtoto mdogo.“Wakati linapata ajali lilikuwa likitokea Mkoa wa Mwanza, hizi ni taarifa za awali, kama kutakuwa na vifo zaidi au majeruhi kuongezeka tutawapa taarifa, maana mpaka sasa polisi wanaendelea na uchunguzi ili kujua pia chanzo cha ajali na idadi ya abiria waliokuwemo” amesema
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger