.

9/12/2021

Wapenzi Wawili Wakutwa Wamefariki Baada ya Kunywa Sumu Kwenye Juice Mlandizi


Watu wawili wamefariki kwa kunywa sumu katika Kitongoji cha Mlandizi kata ya Mlandizi Tarafa ya Mlandizi Wilaya ya kipolisi Mlandizi Mkoani Pwani.

“Tarehe 5 September 2021 asubuhi huko Mlandizi Watu wawili wanaodaiwa kuwa ni Wapenzi walikutwa wamefariki katika makazi yao baada ya kunywa ya kitu kinachodhaniwa ni sumu, Watu hao ni Godfrey Pius Mandai (48) ambaye alikuwa ni Dereva wa Kampuni na Veronica Gerald ( 42) Mfanyabiashara na mkazi wa Mtwara ambaye alisafiri kutoka Mtwara na kumfuata Mpenzi wake huyo Mlandizi.

“Mwanaume yule alitengeneza juisi ambayo ndani yake ilikuwa na sumu akampa Veronica akanywa na kufariki, Mwanaume alipoona Mpenzi wake amefariki na yeye akanywa na akafariki”

“Chanzo ni wivu wa kimapenzi ambapo Mwanaume alikuwa anamtuhumu Veronica kuwa anafanya usaliti, kwenye eneo la tukio tumekuta chupa yenye masalia ya sumu na tumekuta pia karatasi ambayo inadhaniwa imeandikwa na mmoja wao na imeandikwa ‘HUU NI USALITI TU’” ——— asema Kamanda wa polisi Mkoa wa Pwani Wankyo Nyigesa.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger