Ticker

6/recent/ticker-posts

Wasanii Kuanza Kulipwa MIRAHABA Watapata 70%, Serikali 30%.


WAKATI Wasanii wa Tanzania wakisubiri kuanza kulipwa mirabaha ya nyimbo zao kuchezwa kwenye TV, Radio na maeneo mengine yanayotumia muziki kuanzia Dsemba 2021, Ofisa TEHAMA wa COSOTA Segenge James amesema mgao wa pesa Wasanii watapata 70%, Serikali 30%.

"Mgao wa pesa ni Msanii atapata 70% na COSOTA 30%, hizi pesa hazitokuwa zinakwenda kwenye masurufu mengine Serikalini ndio maana imekua 70% tunawapa wao na 30% tunatumia sisi kwa matumizi ya kuturahisishia kufikia maeneo mbalimbali kuwakusanyia wao pesa wanayotakiwa kuipata.

“Wafanyabiashara wataingia hakimiliki.co.tz wataweka taarifa zao za biashara na kupata control number na kulipia leseni ya matumizi ya kazi za muziki, tumefanya kikao na kuwaelimisha Maafisa Utamaduni na Maafisa Biashara ili kuondoa usumbufu na mlolongo usiohitajika." - Ofisa TEHAMA wa COSOTA Segenge James.


Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments