WHO yasema ukosefu wa chanjo Afrika unaweza kuirudisha nyuma dunia

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA





 Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema Afrika inakabiliwa na upungufu wa dozi milioni 470 za chanjo ya Covid-19 mwaka huu, baada ya mpango wa kimataifa wa Covax kupunguza makisio ya shehena yake, na kuibua wasiwasi wa aina mpya na hatari za kirusi hicho. 
Kitengo cha WHO barani humo kilisema katika mkutano wa kila wiki mjini Brazaville hapo jana, kwamba ni asilimia 17 tu ya wakaazi wa bara hilo ndiyo watakuwa wamechanjwa kufikia mwishoni mwa mwaka huu, ikilinganishwa na shabaha ya asilimia 40 iliyowekwa na WHO. 

Mkurugenzi wa WHO Afrika, Matshidiso Moeti, alisema ukosefu wa usawa na upatikanaji hafifu wa chanjo vinatishia kuyageuza maeneo barani Afrika, kuwa maeneo ya kuzalisha virusi visivyosikia chanjo. 

Kutokana na uhaba wa kimataifa, mpango wa Covax utasafirisha karibu pungufu ya dozi milioni 150 kuliko ilivyopangwa. Upunguzaji huu wa malengo ya chanjo unakuja wakati Afrika imevuka mambukizo milioni nane wiki hii, imesema WHO.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad