Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Wizara Yamtambua Aliyetembea Kutoka Kigoma Hadi Kilimanjaro

  

Serikali kupitia Wizara ya Afya imemtambua Mwanariadha Michael Nondo, mkazi wa Kigoma aliyejitolea kutembea kutoka mkoani Kigoma hadi Kilimanjaro kwa lengo la kuelimisha na kuhamasisha wananchi kuchanja chanjo ya COVID-19.

Michael Nondo, aliyetembea kutoka Kigoma hadi Kilimanjaro kwa ajili ya kuhamasisha chanjo ya COVID-19

Katibu Mkuu Wizara ya ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Prof. Abel Makubi, ameelezea wizara kuutambua mchango wa mwanariadha huyo.


"Kama serikali tunatambua juhudi zinazofanywa na wadau mbalimbali katika mapambano haya ya Corona, lakini kwa leo kama Wizara niseme, tumetambua ndugu Michael Nondo, aliyeonesha ujasiri na uzalendo wakutembea kutoka mkoani Kigoma mpaka mkoani Kilimanjaro ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi zinazo endelea nchini kote," amesema Prof. Makubi. 

 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments