Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Air India: Ndege iliyokwama chini ya daraja na kusababisha gumzo mtandaoni
Video ya ndege ya shirika la ndege la India Air India iliyokwama chini ya daraja la mji mkuu, Delhi, imekuwa ikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii.
Ndege hiyo, ambayo inaripotiwa kuwa ilikuwa imeuzwa, ilikuwa ikisafirishwa ndipo ilipokwama.

Video hiyo inaonyesha magari yakipita kando ya ndege hiyo ambayo mbawa zake zinaonekana kung’oka.

Mwandishi wa habari, aliyetuma ujumbe wa twitter, ambaye alishirikisha umma video ya ndege hiyo, alituma pia taarifa ya Air India ambayo ilisema kuwa ndege hiyo haikuwa na uhusiano na kampuni hiyo tena.

"Hii ni sehemu ya ndege ambayo usajiri wake wa kampuni ya Air India uliuzwa. Hii ilikuwa inasafirishwa usiku wa jana na mmoja wa wanunuzi wake wapya.

Air India haina uhusiano wowote na ndege kwa hali yoyote ile ," taarifa hiyo ilisema.

 HABARI KAMA HIZI DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL KWA KUBONYEZA > HAPA

Post a Comment

0 Comments