Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Ajali: Magari Mawili Yateketea Kwa Moto, Chanzo Cha Moto Kinashangaza, Afisa Misitu Afunguka 

Gari aina Nissan Patrol ya Idara ya maji ya Halmashauri ya Mji wa Makambako na semitela mbili zimeungua kwa moto eneo la changarawe mjini mafinga huku chanzo chake kikidaiwa kuwa ni moshi wa moto uliokuwa ukiwaka pembezoni mwa barabara.

 

Akizungumzia tukio hilo Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Saad Mtambule amesema chanzo kilichopelekea magari hayo kuungua ni moshi uliosababishwa na moto uliokuwa ukiwaka pembezoni mwa barabara

 

Aidha Mkuu wa Wilaya amesema tatizo kubwa linaloikumba wilaya ya mufindi kwa sasa ni moto unaoibuka mara kwa mara na kupelekea kuteketeza shamba la miti la serikali pamoja na mashamba ya watu binafsi

 

Kwa upande wake Mhifadhi Mkuu wa Shamba la Miti Sao Hill Lucas Sabida amesema kwa kipindi cha wiki moja zaidi ya ekari 250 za shamba hilo zimeteketea kwa moto Hata hivyo kufuatia ajali ya magari hayo hakuna kifo kilichotokea ambapo horse ya semitela iliteketea kwa moto na gari ndogo aina ya Nissan nayo iliteketea kwa moto


OPEN IN BROWSER

 Downlaod App ya BLOG Hii Kutoka Google Play Kwa Kubonyeza HAPA>>>

Post a Comment

0 Comments