Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Ali Kiba "Sina Mazoea na Shilole na Wala Sikumualika Kwenye Event yangu"
Kwa mara ya kwanza @officialalikiba amefunguka kuhusiana na yote yaliyotokea kwenye Listening Party ya albamu yake iliyofanyika Serena Hotel tarehe 6 ya mwezi huu jijini Dar es salaam hasa likiwepo suala la @esha.s.buheti alichokileta mitandaoni.

Akiwa kwenye XXL ya @cloudsfmtz ,Alikiba amedai alishangazwa na kitendo cha Esha na kilimghafirisha sana maana tokea siku ya kwanza anamchukulia Esha kama familia yake, wanaongea kila kitu viwe vitu vya maana hata vya kishenzi lakini cha ajabu uwenda haoni thamani ya kumuweka karibu na familia yake akataka zaidi amtaje na ajabu sana mitandao ya kijamii ndio imeharibu hili. Alikiba pia amedai kuna watu wengi wanafanya kazi zake sana na aliwasahau kuwataja sababu ya furaha aliyokuwa nayo siku hiyo mfano mtu anayedili na social networks zake,Capacitor,Meneja wake Aidan.

Kuhusu mualiko wa @officialshilole ,Alikiba amedai hana mazoea na Shilole hata kidogo na wala hakumualika kwenye event hiyo,alishangaa tu Shilole yupo pale maana hata ingekuwa ni kumtaja hasingeweza kumkumbuka abadani maana hawana mazoea. Na alisikia kuwa masuala ya chakula uwenda ndio ikawa sababu ya Esha kufanya vile, hilo suala halipo.


 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments