Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Vanessa Amfariji Wema Sepetu
VANESSA Mdee ndiye mama mpya mjini! Nddiyo, siku chache baada ya kutangaza ujauzito wake mkubwa, ni rasmi sasa kwamba amejifungua mtoto wa kiume.

 

Mastaa kutoka kada mbalimbali Bongo wamempongeza Vanessa ambaye alikuwa msanii mkali wa Bongo Fleva akiwemo mwigizaji Wema Sepetu ambaye ameweka wazi kwamba anamuonea wivu kwa kujaaliwa mtoto.

 

Wema amekuwa akieleza mara kwa mara jinsi ambavyo suala la kukosa mtoto linamtesa hasa baada ya kufikisha umri wa miaka 30 na kuendelea ambapo wiki hii alifikisha umri wa miaka 31 (kwa mujibu wake yeye mwenyewe).

 

Hata hivyo, baada ya kuona ‘komenti’ yake, Vanessa amemfariji kwa kumwambia muda unakuja naye atapata mtoto na atatoa ushuhuda mzuri.

 

“Siku moja utatoa ushuhuda mzuri na utakuwa na mtoto…” Vanessa amemfariji Wema.

Wema amekuwa na aibu ya kuzungumzia suala la kukosa mtoto kutokana na namna anavyoshambuliwa na baadhi ya watu wakimwambia kwa umri wake alipaswa kuwa na mtoto.

 

“Ningekuwa na uwezo wa kuzaa ningekuwa nimezaa kitambo sana, lakini siwezi. Simlaumu Mungu kwa hali niliyonayo. Je, napaswa kuwaambia kila siku ni kwa jinsi gani ninateseka na kuumia kwa kukosa mtoto wangu mwenyewe?” Wema aliwahi kulihoji gazeti hili la IJUMAA baada ya kuona kama linamuandama juu ya ishu hiyo na kuongeza;

 

“Unajua mimi nilikuwa na tatizo kubwa sana kwa upande wa tumbo langu la uzazi lililosababisha nisiweze kuzaa kwa muda wote huu.

 

“Ngoja niweke wazi watu wajue, mimi nina ugonjwa ambao unasababisha mayai yangu ya uzazi kutoboka na kushindwa kupevusha mbegu za uzazi.”

STORI; KHADIJA BAKARI, DAR

 HABARI KAMA HIZI DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL KWA KUBONYEZA > HAPA

Post a Comment

0 Comments