Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Alikamwe "Mambo 10 nilioyaona YANGA Ikimtandika Kimoko GEITA1: Bado kuna Yanga mbili zisizofanana kiwanjani.. Dakika 45 za kwanza inakuburisha.. Dakika 45 zinazofata, inakushangaza! Jambo jema kwa WANANCHI, Bado Timu imebeba Pointi 3 katika Perfomance ya kawaida

2: Ni mapema kusema Lolote kwa Geita, Lakini ni kwa haraka sana wanatakiwa kuzinduka kutoka usingizini. Uwezo wao bado uko chini mno kushindana kwenye TPL

3: Nafikiri Nabi hana imani sana na Mauya kiasi cha kukubali kumtoa Feisal kama namba 10 ili Aucho aweze kucheze namba 6! FeiToto akiwa namba 8 kuna kitu kinapungua kwenye system ya Yanga

4: Nabi asiendelee kutudanganya. Yanga inakata upepo! Vifua vya wachezaji vinakata upepo mapema. Si mara zote utacheza na Quality kama ya Geita!

5: Mastraika wa Yanga wanatakiwa kuongeza ukatili mbele ya Lango. Zile dakika 45 za kwanza, Timu ikiwa na Energy ya kutosha, wanatakiwa kutumia vyema zile nafasi kumaliza mchezo

6: Juma Mahadhi anatakiwa kusimama na kuonyesha tofauti ya uzoefu wake kuisaidia Geita. Bado anacheza kama ameshafanya kila kitu kwenye soka! Geita bado inamuhitaji sana

7: YANICK BANGALA..🙌 Katika 'pumzi' ile ya timu, unahitaji Mwanaume mmoja pale nyuma kusimama na kulinda heshima ya klabu. Bangala anawapa Yanga usingizi mzuri hata wakiwa na siku mbaya kazini

8: Yacouba Sogne! Yes, pasi nzuri ya bao kwa Moloko, Lakini bado hawezi kutoka na tabasamu kiwanjani. Ana papara mno! Kuna presha na uchoyo unaomfanya awe na maamuzi yasio sahihi mara nyingi

9: Kuumia kwa Danny Lyanga kulimpa nafuu kiasi Dickson Job! Geita walipoteza mwanaume imara kwenye safu ya ushambuliaji katika nyakati muhimu zaidi kiwanjani

10: Farid bado hajawapa Yanga wanachokisubiri kwake! Well done Kibwana Shomari.. mwisho wa siku, 'Line 2' kamnyima Mayele bonge la Bao!

Nb: Bila yule Ostaz, ni Ndanda ya Mjini 😀

 Downlaod App ya BLOG Hii Kutoka Google Play Kwa Kubonyeza HAPA>>>

Post a Comment

0 Comments