Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Amuuwa Mke kwa Panga Kisa Wivu wa Mapenzi

 
Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Regina Jiyenze mwenye umri wa miaka 45 mkazi wa Mtaa wa Mbulu wilayani Kahama mkoani Shinyanga, ameuawa na mumewe Heneriko John kwa kukatwa na panga kichwani na begani na kupoteza maisha papo hapo akiwa nyumbani kwa balozi.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga George Kyando, amesema tukio hilo la mauaji limetokea leo majira ya saa 3:45 asubuhi wakati mwanamke huyo alipokwenda kutoa taarifa kwa balozi wa mtaa wake juu ya kutishiwa kuuawa na mumewe na ndipo mumewe huyo alimvamia akiwa ameficha panga na kumkata.

Kamanda Kyando amesema chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa mapenzi kutokana na mtuhumiwa kudai mke wake alikuwa siyo mwaminifu kwenye ndoa yao, kitendo ambacho kilimsukuma kuamua kufanya mauaji hayo ya kikatili.


 HABARI KAMA HIZI DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL KWA KUBONYEZA > HAPA

Post a Comment

0 Comments