Ticker

6/recent/ticker-posts

Ashambuliwa na Kundi la NYUKI Akichepuka na Mke wa Mtu


Mwanaume mmoja amenusurika kifo baada ya kuvamiwa na kushambuliwa na nyuki waliomuachia majeraha wakati akichepuka na mke wa mtu.

Inadaiwa mwanaume huyo kabla ya kukumbwa na mkasa huo alikuwa ameonywa na mwenye mke.

Mwanaume huyo Jethro Maimba kutoka kijiji cha Kwaramba katika mji wa Gokwe uliopo katika jimbo la Midlands nchini Zimbabwe anadaiwa siku ya tukio alikuwa akichepuka na mke wa mtu aitwaye Lizzie Maphosa na wakati wanaendelea na tendo hilo ghafla kulitokea kundi la nyuki ambalo lilimshambulia vikali na kumuacha akiwa hoi taabani.

Mashuhuda wa tukio hilo wanasema bwana Maimba alipewa onyo mara kadhaa na mume wa mwanamke huyo Joseph Musariri na bado hakusikia hadi hapo alipovamiwa na kundi la nyuki.

Mahakama ya jadi iliyo chini ya Chief Nemangwe wa eneo hilo baada ya kusikiliza shauri hilo iliwataka wahusika warudi nyumbani wakalishughulikie kifamilia na kuondoa tofauti zao.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments