Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Bernard Membe "Musiba Popote Ulipo Naomba Hela Zangu"


“Niwaambie Watanzania wenzangu hakuna Mtanzania awe Ndovu au sisimizi mwenye kusimama juu ya sheria hakuna aliye juu ya sheria, ukimdhalilisha mwenzako ukadhani kwamba utaendelea kupiga miluzi na kufurahia kana kwamba wewe umefika Duniani kama Kiongozi au ndio mkubwa au Mungu Mtu, Mahakama Kuu ni jibu kwamba ukidhalilishwa fika Mahakamani uitafute haki yako nimefika hapa kwa niaba ya watanzania wote na Viongozi Wastaafu walionyanyaswa na kudhalilishwa na Mtu huyu"

"Naomba wajue hili halitotokea tena, hasimami tena kudhalilisha Wazee na Viongozi wake, hasimami tena na kujifanya yeye ni Mungu Mtu, hasimami tena kuwatukana Watu walioifanyia kazi Nchi hii kwa uaminifu na uadilifu wote, anasimama Mtu kwa kutumwa na kulipwa akadhani kwamba ataendelea kuishi Duniani katika hali hiyo hamtomuona tena akifanya hivyo na Musiba huko uliko naomba hela zangu" ——— Bernard Membe baada ya kushinda kesi Mahakama kuu dhidi ya Musiba ambapo Mahakama imeamuru Musiba amlipe Bilioni 6 kwa kumchafulia jina. #MillardAyoMAHAKAMANI

 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments