Ticker

6/recent/ticker-posts

CCM yampongeza Rais Samia Suluhu mkopo wa trioni 1.3 fedha za UVIKO 19 kutekeleza miradi

Chama cha Mapinduzi Taifa CCM kimempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  kwa kufanikisha mkopo wenye masharti nafuu wa dola milioni 579 sawa na sh. trilioni 1.3 za Kitanzania  kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya mipango ya kimaendeleo kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF).

 

Sambamba na hilo CCM imewataka viongozi  wa Kamati za siasa za chama hicho kuanzia ngazi ya shina hadi Mkoa kusimamia kwa karibu matumuzi  ya fedha hizo na ziende kutumika kama ilivyokusudiwa.

 

Akizungumza na vyombo vya habari Jijini Dodoma leo Octoba 12, 2021 Katibu wa Itikadi na uenezi wa chama cha mapinduzi CCM Taifa amesema Rais Samia ameendelea kulinda tunu za taifa huku akihakikisha maendeleo endelevu yanapatikana kwa serikali na hata kwa mtu mmoja mmoja. 

 

Shaka amesema Mkopo huo ni fursa muhimu kwa watanzania kwani mkopo huo umepatikana wakati bajeti ya serikali  ikiwa imepita hivyo hakuna litakalo teteleka kutokana na kupata kwa mkopo huo.

 

"Tukumbuke kwamba fedha hizi sio sadaka ni fedha kwa ajili ya Maendeleo ya watanzania ambapo zikitumika vizuri uchumi wa nchi utakuwa zaidi na hata wananchi mmoja mmoja wanakwenda kunufaika,

 

"hivyo basi Chama kinaomba kuendelea kumuunga mkono Rais wetu kwani ameonekana kuwa na mapenzi mema kwa nchi na wananchi wake kwa ujumla ,"amesema Katibu huyo Shaka.

 

Aidha Bw. Shaka Hamdu Shaka ameziagiza kamati za siasa za Mikoa hadi ngazi ya shina kuhakikisha fedha hizo zinatumika ipasavyo kwa kuwa chama ndio wasimamizi wa serikali hivyo wanawajibu wa kuhakikisha waliyoahidi yanatekelezeka.

Katika hatua nyingine amewapongeza na kuwashukuru wananchi na wanachama wa wa Jimbo la Ushetu Mkoa wa Shinyanga  kwa kukipa ushindi wa kishindo katika uchaguzi huo pia wamekipongeza cha cha ACT Wazelendo kwa kuibuka na ushindi jimbo la Konde Zanzibar.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments