Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Chawa wa Diamond Platnumz Baba Levo Avutiwa na Ali Kiba


@officialbabalevo ni chawa mkubwa wa @diamondplatnumz lakini ameshindwa na siku zote anashindwa kuvumilia kuficha hisia zake juu ya mapenzi yake ya dhati kwa Alikiba, kiukweli Babalevo anamkubali sana Alikiba, hivyo haoni tabu kabisa kumpost kwenye page zake ingawa anatoka katika upande wa pili( WCB)

Baba levo ameipenda sana ngoma ya "niteke" kutoka katika album ya kingkiba, hilo limethibitika baada ya yeye mwenyewe kupost kwenye page yake instagram.

Inaonekana kabisa kuna watu wako WCB Lakini wanampenda sana Alikiba, ila kwasababu wanamuogopa big boss basi wanaficha hisia zao. Pia wengine ni wasanii na wamevutiwa na Album hiyo lakini wanaogopa kupost Album ya alikiba maana wako karibu na WCB, Hivyo wanaogopa connection isikatike kule kwa BROO BIG.

BABA LEVO KAIKUBALI NITEKE, VIPI WEWE UNAIKUBALI NGOMA GANI KUTOKA KWENYE ALBUM YA ALIKIBA?

 HABARI KAMA HIZI DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL KWA KUBONYEZA > HAPA

Post a Comment

0 Comments