Ticker

6/recent/ticker-posts

EDO Kumwembe "Please Respect Mbwana Samatta, Respect Our Captain Acheni Nongwa"


Edokumwembe Ameandika haya:

"PLEASE RESPECT SAMATTA...RESPECT OUR CAPTAIN....Nasikia maneno mengi kuhusu Samatta halafu huwa nasononeka sana moyoni... Ndani ya uwanja Kule Ulaya Samatta anasimama kati pale mbele akivizia...huku timu yetu ya taifa anahangaika kufanya mambo mengi uwanjani...atoke deep, aunganishe timu ajaribu kufunga....Samatta asipofunga huwa ni nongwa..kwa mfano hizi game mbili hajafunga na ni nongwa kubwa.....akifunga Msuva na mchezaji mwingine huwa tunawaona kama vile sio Watanzania. Guys Msuva ni staa mkubwa na anacheza Waydad Casablanca..akifunga yeye na asipofunga Samatta ni kitu kile kile tu. Ni sawa pale Argentina asifunge Messi halafu afunge Di Maria..Hivi tunamchukuliaje Msuva? .tunaporudi kwa Samatta tusimkosee heshima...amewafanya watoto wetu waamini ni kweli kwamba kumbe kuna Mtanzania aliyezaliwa uswahilini Tanzania anaweza kucheza Ubelgiji, England, Uturuki katika high level...amewafanya vijana wetu waamini katika ndoto zao. Ni kitu kikubwa katika maisha yetu kwa sasa pengine kuliko matokeo ya Taifa Stars kwa sababu hao wenye ndoto ya kuwa Samatta ndio ambao watatutengenezea Stars imara zaidi kuliko ya leo...nawakumbusha tu wanaomdharau Samatta leo kwa sababu ya mihemko ya kwamba kila mechi ya Stars lazima afunge bila ya kujali aina ya wachezaji anaocheza nao....Samatta ni Mtanzania wa kwanza kuchukua ubingwa wa Afrika, Mtanzania wa kwanza kuwa mfungaji bora Ligi ya Mabingwa wa Afrika, Mtanzania wa kwanza kuwa mwanasoka bora wa ndani Afrika, Mtanzania wa kwanza kucheza Ligi Kuu Ubelgiji, Mtanzania wa kwanza kufunga mabao mengi Ubelgiji, Mtanzania wa kwanza kuuzwa pesa nyingi Ulaya, Mtanzania wa kwanza kucheza Ligi Kuu ya England. Mtanzania wa kwanza kufunga bao Ligi Kuu ya England, Mtanzania wa kwanza kuzifunga Liverpool na Manchester City na Wembley.Mtanzania wa kwanza kucheza katika Ligi kuu ya Uturuki na klabu kubwa Uturuki. Kuna rekodi nyingi ambazo hazitafutwa. Kabla ya kuhoji uzalendo wa Samatta lazima tujiulize ni lini aligoma kuja kuichezea tmu ya taifa tangu akiwa na TP Mazembe, Genk, Aston Villa, Fenerbahce na sasa Royal Antwerp ya Ubelgiji. Mara zote amekuwa akipaatikana. Unajua anatumia saa ngapi hewani kwa mwaka kurudi kuichezea hii timu...LEGEND" 

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments