Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Esha Buheti "Mume Wangu Anajua Nampenda Alikiba, Sitaki Kumpoteza"
Muigizaji wa filamu na Mfanyabiashara Esha Buheti amesema mapenzi aliyonayo kwa Mwanamuziki Ali Kiba ni makubwa sana na hatamani hata kumpoteza kwani ni kama mdogo wake.Akizungumza kwenye Kipindi cha Lavidavi cha Wasafi FM, Esha amesema kwamba kuna wakati anajitoa kwa ajili ya Mwanamuziki huyo hadi mumewe anabki kushangaa kama yote hayo ni kwa aji ya Kiba tu.

Akiendelea kueleza upendo wake kwa Mfalme huyo wa Bongo Fleva Esha anasema aliwahi kufunga safari mpaka Mombasa kwenye harusi ya msanii huyo huku akimuacha mtoto wake nyumbani akiwa na miezi sita tu tangu kuzaliwa.

Akizungumzia kuhusu sintofahamu aliyoizua masaa machache baada ya Kiba kuachia Albam ya ‘Only One King’ Esha anasema tayari matatozo yao yamekwishamalizika na asingependa kuongelea zaidi.

“Nampenda sana Ali. Mtu unayempenda unakua hutamani kumpoteza. Mume wangu anajua ninavyompenda mpaka kuna wakati anauliza haya yote ni kwa ajili ya Ali tu? Nilienda Mombasa na kumuacha mwanangu mwenye miezi sita na Bibi yake. Hiyo yote ni ‘Love’ iliyopo ndani yangu” Esha.

Kabla na mahojiano hayo, King Kiba aliweka mambo sawa kwenye mtandao wa Instagram ambapo alimtaka Esha ajue namna gani anathamini mchango wake na hata kumchukulia kama dada na familia kwake.

BY : Fatuma Muna

 Downlaod App ya BLOG Hii Kutoka Google Play Kwa Kubonyeza HAPA>>>

Post a Comment

0 Comments