Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Fally Ipupa "Nimekuja Tanzania Kuonesha Ukubwa wa Muziki"

 


Mwanamuziki maarufu wa muziki wa dansi na Rhumba Fally Ipupa wakati amesema  amejiandaa kutoa burudani kwa Watanzania katika ukumbi wa Mliman City jijini Dar es Salaam.

Amesema hayo leo Oktoba 8,2021, mwanamuziki huyo aliyejizoelea umaarufu kwa staili ya kucheza na kuimba, amewaambia waandishi wa habari kilichomleta Tanzania ni matukio mawili ya burudani, moja litakalofanyika Mliman City Oktoba 9 na pili katika ukumbi wa Malaika jijini Mwanza Oktoba 13 mwaka huu

"Njooni mshuhudie burudani,mimi na wanamuziki wenzangu ambao nimekuja nao tumejiandaa, kwa wale wa Dar es Salaam na maeneo jirani tukutane Mliman City na kisha tutakwenda Mwanza,"amesema Fally Ipupa ambaye umaarufu wake umevuka mipaka ya bara la Asia na Amerika ukiachilia Bara la Afrika ambako amejizolea umaarufu mkubwa sana.

Wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari waliotaka kufahamu amekuwa akivutiwa na wasanii gani wa Tanzania amejibu wako wengi lakini baadhi yao ni Diamond, Ali Kiba ,Barnaba ,Nandy huku akiweka wazi yupo katika mchakato wa kufanya wimbo na Ali Kiba baada ya kuimba na Diamond.

"Baada ya kufanya vizuri katika kibao cha 'Inama' na msanii  Diamond Platnumz  sasa ni zamu ya AliKiba na wasanii wengine,mimi sibagui, "amesema Fally Ipupa wakati akizungumzia wimbo huo wa 

Inama uliotoka miaka miwil iliyopita na mpaka sasa umeshatazamwa mara milioni 98 katika mtandao wa Youtube.

Ameongeza wimbo huo ni  kweli wimbo umepokea vizuri na yote haya ni kutokana  na uzuri wa wimbo wenyewe kuanzia biti mpaka mashairi.

Kwa upande wake Mratibu, wa kampuni ya Prime Time Promotions,waliomleta mwanamuziki huyo, Edward Lusala amesema katika show hiyo mbali na Ali Kiba pia kutakuwa na wasanii wengine ambao ni 'Suprise'.

"Nawashauri watu kujitokeza kwa wingi kwa kuwa ndio watakuwa wa kwanza kuonja utamu wa albamu ya sita ya msanii huyo kwa nchi za Afrika ambapo hii ni mara yake ya kwanza kuifanyia show,"amesema huku akisisitiza kila kitu kuelekea katika Show kimemilika.

 HABARI KAMA HIZI DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL KWA KUBONYEZA > HAPA

Post a Comment

0 Comments