Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Harmo Anakunywa Pombe Kamili Mwanawe Togwa

HARMONIZE ni baba wa mtoto mmoja wa kike aitwaye Zulekha au Zuu ambapo mama wa mtoto huyo amemtumia mkeka wa matumizi ya mtoto.

 

Mama Zuu ameorodhesha vitu kedekede ambavyo Harmonize anatakiwa atume, lakini amekuwa hatumi katika wakati huu akiwa nchini Marekani kwa ajili ya ziara ya kimuziki.

 

Vipo vitu vingi ambavyo Mama Zuu ameorodhesha; vingine ni sawa na vingine vimeacha baadhi ya watu midomo wazi.

 

Baadhi ya mashabiki wake walioona mkeka huo wamemshambulia Harmonize kwenye kurasa zake za kijamii wakimwambia yeye huko Marekani anakunywa pombe kamili, lakini mwanawe Zuu anakunywa togwa.

 

Mashabiki hao wamesema kuwa, mahitaji hayo ni ya kawaida kabisa amabyo Harmonize anatakiwa kumtimizia mwanawe kuliko kuendelea kuringishia madola na vito vya thamani wakati hatoi matumizi ya mtoto na kumuachia majukumu mama wa mtoto pekee.

 

Kwa upande wake Harmonize amesambaza ujumbe huo wa kutakiwa kutoka matumizi ya mtoto kutoka kwa mzazi mwenzake huyo ambaye walishamwagana. Harmonize ambaye anaendelea kukiwasha huko Marekani aliweka mkeka huo kwenye Insta Story yake na kuandika;

 

“Anaitwa anaitwa Mama Zuu pale anapoona unachelewesha mahitaji kwa kisingizio upo Marekani kutuma hela ni ngumu anashusha mkeka…!!!” Hata hivyo, Harmonize ameeleza kuwa hoi na mjumuisho wa vitu kama chama za watoto katika orodha hiyo.

 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments