Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Hatimaye Kanye West Amebadili Jina Lake Kisheria, Kwa Sasa Kutambuliwa Kwa Jina Hili
Kutoka Los Angels Marekani, Hakimu aliyekuwa akisimamia suala la Rapa Kanye Omari West, kubadili jina lake kisheria na Kuitwa Ye, tayari amethibitisha na kulimaliza Suala hilo.

Ye ndio Jina litalokuwa likisomeka kwenye nyaraka zote za Kanye West kuanzia sasa bila kuwa na jina la kati wala la mwisho.

@kanyewest alijaza nyaraka za kubadili jina kisheria (deed poll), August 24 mwaka huu huku akidai anafanya hivyo kwa sababu zake binafsi.

Pia Kanye West ameingia kwenye headlines baada ya kuonyesha staili mpya ya nywele zake (Hair cut) staili ambayo ni ya ajabu ila kama ilivyo kawaida kwa Ye ni kutaka utofauti siku zote.

 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments