Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Hizi Hapa Sababu za Chama Cha Chadema Kupigwa Block Kumuona Mbowe
Baadhi ya makada wa Chadema waliofika kumuona Mwenyekiti wao, Freeman Mbowe juzi katika gereza Ukonga jijini Dar es Salaam, hawakutimiza lengo lao baada ya askari Magereza waliokuwa getini kuwazuia wakisema kuwa wamepata maelekezo kutoka juu.
Hata hivyo, Msemaji wa Magereza Kamishna Msaidizi, Justin Kaziulaya alipoulizwa kwa simu jana alikiri kuwazuia akisema ni kutokana na idadi yao kuwa kubwa jambo alilosema linaakiuka masharti ya kupambana na maambukizo ya Uviko-19.

“Ukiangalia kwa haraka haraka picha za watu walioenda kumuona Mbowe jana, Mkuu wa Gereza alikuwa anatekeleza maagizo ambayo yanafuatwa kwa magereza yote nchini na sio kwa mhalifu fulani,” alisema.

Mbowe alikamatwa Julai 30 jijini Mwanza na kuunganishwa na wenzake watatu katika kesi inayohusisha kupanga njama za kufanya ugaidi inayoendelea kusikilizwa na Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia taarifa hizo kwa simu, Mkurugenzi wa Uhusiano, Itifaki na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema alisema hatua ya kuwazuia kumwona Mwenyekiti wao inazua hofu kuhusu hali yake.


 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments