Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Hukumu ya Sabaya Kutolewa Leo, Macho na Maskio yote Leo ArushaHukumu ya kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wialaya ya Hai Lengai ole Sabaya na wenzake wawili Silvester Nyegu na Daniel Mbura inatarajiwa kutolewa leo Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.


Lengai Ole-Sabaya (mwenye suti ya bluu) na washtakiwa wenzake wakiwawamefika mahakamani leo.
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Amalia Mushi aliahirisha hukumu hiyo Oktoba Mosi, 2021 baada ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Odira Amworo, kutokamilisha kuandika hukumu hiyo.

Agosti 12 watuhumiwa hao walielezwa kuwa wana kesi ya kujibu baada ya kukamilika ushahidi wa mashahidi 11 wa Jamhuri na vielelezo vinane.

Sabaya alisimamishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Mei 13, 2021 na Rais Samia Suluhu a ili kupisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali zilizokuwa zinamkabili.

BY: Fatuma Muna

 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments