Ticker

6/recent/ticker-posts

Huu Ndio Ulimwengu Tunaoishi, Mauzo ya Nyimbo za R Kelly Yapanda Mara Dufu
Dunia ina mambo,mtu akifa au kupata tatizo basi atafwatiliwa zaidi kuliko akiwa kawaida. Hii imetokea kwa msanii mkongwe wa R&B duniani tokea pande za Marekani, R.KELLY ambaye mwishoni mwa mwezi wa tisa alikutwa na hatia ya mashtaka saba yaliyokuwa yakimkabili likiwemo shtaka la biashara ya ngono na hukumu yake ikisubiriwa tarehe 4 mwezi wa tano mwaka 2022.

Inawezekana R.kelly akawa ameanguka ila muziki wake bado unaenda juu zaidi. Unaambiwa ndani ya wiki moja tokea kesi yake isomwe na kukutwa mwenye hatia,mauzo ya muziki wake yamekuwa yakipanda maradufu. Kuanzia September 27th hadi October 3rd mauzo ya Audio zake yalipanda kwa 22% huku video zake zikiuza kwa 23%.

Streams zake zimepanda tokea milioni 11.2 hadi milioni 13.14 ma mauzo ya Albamu zake yakipanda hadi 500%.

Inaonesha zile kampeni za Stop streaming R.kelly na Mute R.kelly zikimezwa na mapenzi ya mashabiki wa muziki wake,baada ya tukio hili la Mauzo ya muziki wake kupanda,hisia nyingi za watu mitandaoni ni FREE R.KELLY huku kila mmoja akiambatanisha sababu zake.


Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments