Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Jide Naye Kupumzika Muziki
MWANAMUZIKI mkongwe kunako tasnia ya muziki wa Afro-Pop, Lady Jaydee au Jide anasema kuwa, anafikiria kupumzika muziki huo hadi mwaka 2024.

Utakumbuka Februari 12, mwaka huu, Jide alizindua albam yake mpya ya nane tangu aanze muziki ambayo ameipa jina la 20 kama sehemu ya kuhadhimisha miaka yake 20 aliyofanya muziki.

Jide amesema; “Nafikiria kuchukua zangu break hadi 2024…”

Kisha ameongeza; “Nikaishi maisha tofauti na haya niliyoishi kwa miaka 21. Kila mtu anahitaji break maishani ama?”

Hadi kufikia sasa, Jide ameachia albam kama Machozi (2001), Binti (2003), Moto (2005), Shukrani (2007), The Best of Lady Jaydee (2012), Nothing But The Truth (2013), Woman (2017) na 20 (2021).

Jide anatangaza uamuzi huo ikiwa ni mwaka mmoja tangu msanii mwingine wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee alipotangaza kusimama kufanya muziki.


 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments