Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Kamanda Amefunguka Juu ya Gari Ambalo limetumbukia Katika Bahari Coco Beach


Kamanda wa Polisi Mkoa wa kipolisi Kinondoni, Ramadhani Kingai amefunguka juu ya gari aina ya Toyota Land Cruiser Prado ambalo limetumbukia katika Bahari ya Hindi eneo la ufukwe wa Coco.

Kamanda Ramadhani Kingai kwenye mahojiano na Gazeti la Mwananchi leo Oktoba 5, 2021 amesema hakuna madhara yoyote yaliyotokana na ajali hiyo baada ya mtu huyo (DEREVA) kuokolewa.

Amesema wanasubiri afya yake iimarike ili wafanye uchunguzi wa tukio hilo kwa kuwa dalili zinaonyesha alikuwa ni mtu mwenye mawazo au tatizo la akili.

"Kule alipokuwa anakwenda kulikuwa hakuna barabara, kama mtu ni mzima huwezi kuona gari linakwenda baharini na wewe ukazidi kukanyaga mafuta," amesema Kingai akiliambia Mwananchi.

Wakizungumzia tukio hilo mashuhuda wanadai tukio hilo lilitokea jana saa saba mchana baada ya kuliona gari kwenye maji na alikuwepo dereva pekee ambaye walifanikiwa kumuokoa na kumkimbiza hospitali baada kunywa maji mengi katika jitihada za kujiokoa.

Chanzo: Mwananchi

 HABARI KAMA HIZI DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL KWA KUBONYEZA > HAPA

Post a Comment

0 Comments