Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Kauli ya bosi TTCL kuhusu shirika kuwa na deni la Sh403 bilioni

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Waziri Kindamba amesema faida au hasara ni matokeo ya mauzo ukitoa gharama za uendeshaji wa biashara na kwamba hapo ndipo linapozaliwa gawio.
Kindamba ametoa ufafanuzi huo wakati kukiwa na mjadala mitandaoni kuhusu namna mashirika ya umma yanayokabiliwa na madeni yalivyoweza kutoa gawio kwa serikali licha ya madeni yao.

Siku mbili zilizopita, Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kusema TTCL limelemewa na deni la Sh403 bilioni ilhali mtaji ilionao ni wa Sh243.

"Kwa kuwa kulikua na faida sheria inataka utoe gawio," amesema Kindamba.

 Pamoja na kuelemewa na deni, shirika hilo limekuwa likitoa gawio kwa Serikali.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter leo Ijumaa Oktoba 22, 2021 Kindamba ameandika “ Ratio inayoitwa ‘Debt to Equity’ ratio kiuhasibu haizuii taasisi au kampuni kufanya FAIDA na haina uhusiano na Hasara pia,na haimzuii mwenye Mali (Serikali)kuongeza Mtaji ili kuboresha Equity yake ndani ya taasisi. Maana kwenye liabilities inajumlisha Madeni yasiyoiva na yaliyoiva.”

“Na kwa kua kutoa gawio ni takwa la kisheria Faida au Hasara ni matokeo ya Mauzo yako ukitoa gharama zako za uendeshaji ndani ya mwaka husika wa kibiashara na hapo ndipo linapozaliwa Gawio au kinyume chake, na kwa kuwa kulikua na Faida sheria inataka utoe gawio. Asante” Kindamba.

 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments