Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Kesi ya Mbowe, wenzake kuendelea leo
Kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu, wanaokabiliwa na mashtaka ya ugaidi inatarajiwa kuendelea tena leo Ijumaa Oktoba 29, 2021 katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.
Leo Shahidi wa tatu wa upande wa mashtaka anatarajiwa kupanda kizimbani kutoa ushahidi wake.

Mpaka sasa washtakiwa wameshafikishwa mahakamani na wako mahabusu wakisubiri kuingizwa mahakamani.

Mawakili wa pande zote, yaani Waendesha mashtaka (mawakili wa Serikali) na mawakili wa utetezi wameshafika mahakamani na baadhi ya mawakili wa utetezi wameshaingia katika ukumbi wa mahakama pamoja na wanahabari na wasikilizaji.

Bado waendesha mashtaka bado wako ofisini kwao wakijiandaa.


 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments