Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Kutunza Pesa na Kuzitupa Chini ni Kosa la Jinai
Wizara ya Katiba na Sheria imewatahadharisha baadhi ya watu ambao wanatupata fedha chini wakati wa kutoa zawadi kwenye sehemu zozote za tafrija, kwani kwa kufanya hivyo ni kosa kisheria na atakayekamatwa kwa kufanya kosa hilo atashtakiwa kwa kufanya kosa la jinai.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi, wakati akiongea na wazazi, wanafunzi pamoja na walimu wa shule ya sekondari ya Kilimo Kilosa mkoani Morogoro ambayo ni elimu jumuishi.

“Nadhani wengi hamfahamu, kutupa, kuikunja au kuichana fedha ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kosa la jinai, acheni kutupa fedha, fedha sio karatasi tena ina alama ya Baba wa Taifa, maana yake unamtupa Baba wa Taifa chini?” amesema Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Katiba na Sheria.

 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments