Ticker

6/recent/ticker-posts

 



.

Majaliwa "Samia Tena 2025"





WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema mwaka 2025 Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitampeleka kwa wananchi mtu mmoja, Rais Samia Suluhu Hassan hivyo mawaziri watambue hilo.


Majaliwa ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Oktoba 29, 2021 katika ukumbi wa St Gasper jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa mawaziri na naibu mawaziri.


Majaliwa amewataka mawaziri na naibu wao kuwa wasemaji wakubwa wa mafanikio ya Serikali ili itakapofika 2025, Samia Suluhu Hassan (Rais) apite na kusema kidogo tu.


“Wambieni wananchi kuhusu mazuri yanayofanywa na Serikali hii, tambueni msimamo na mtazamo wa Rais ili mkawe wasemaje zaidi yeye akija awe na maneno machache ya kueleza,” amesema.


Waziri Mkuu amewataka mawaziri na naibu wao kufanya kazi kwa mashirikiano na kuheshimu kauli za viongozi wakuu kwani siyo kila agizo lazima waandikiwe barua ndipo watekeleze.


Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amewataka viongozi hao kuwa mfano kwa mienendo yao wakianzia na mavazi, kauli na kutojiinga katika mambo yatakayowafanya wajadiliwe.


Amesema katika mitandao ya kijamii wapunguze kuzungumza mambo mengi ili kusudi wanapotamka mambo machache yaonekane kuwa na maana kwa jamii.

 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments