Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Manowari ya Marekani yaharibika baada ya kugongana na ‘’kitu kisichojulikana’’

Jeshi la majini la Marekani limesema kuwa manowari yake ya kijeshi inayoendeshwa kwa nguvu za nyuklia iliharibika baada ya kugongana na kitu kilichokua chini ya maji karibu na bahari ya kusini mwa Uchina.
Hatahivyo jeshi hilo la majini halikufichua taarifa zaidi, ambapo lilisema tu kwamba nyambizi hiyo ‘’USS Connect Cut’’ ilikuwa salama na hakikusababisha uharibifu mkubwa.

Haijawa wazi ni kitu gani kilichoigonga manowari hiyo, ambayo kwa sasa inaelekea katika ngome ya Marekani iliyopo kwenye kisiwa cha ‘’Guam’’, ambacho ni eneo la Marekani na ni moja ya maeneo muhimu ya mkakati wa kijeshi wa Marekani katika kanda ya Pacific 

 HABARI KAMA HIZI DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL KWA KUBONYEZA > HAPA

Post a Comment

0 Comments