Ticker

6/recent/ticker-posts

Maskini.. Mtalii wa Ujerumani Afariki Katika Mkasa wa Moto Ndani ya Boti Afrika Kusini

Mtalii wa Ujerumani na mfanyikazi wamefariki dunia baada ya boti ya kifahari ya nyumba kuwaka moto kwenye bwawa katika mkoa wa KwaZulu-Natal nchini Afrika Kusini, ripoti ya vyombo vya habari vinasema nchini humo.
Abiria watano na wafanyakazi wanne wa boti walikuwa ndani ya boti hiyo iliposhika moto katika bwawa la Jozini Jumamosi.

“Wote waliruka ndani ya maji na kwa bahati mbaya watatu kati yao walifariki, miili miwili imeopolewa majini," msemaji wa polisi alinukuliwa akisema na tovuti ya IOL.

Shughuli ya kuwatafuta wafanyakazi wengine waliotoweka inaendelea.

Mamlaka ya Usalama baharini Afrika Kusini (Samsa) imesema inachunguza chanzo cha moto huo.

Boti hiyo iliripotiwa kuwa kwenye safari ya usiku wa pili ilipowaka moto, Samsa imesema.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments