Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Metacha, Makapu Waanza Vizuri Timu ya Polisi Tanzania

NYOTA wa zamani wa Yanga, Metacha Mnata na Saidi Juma Makapu, wameanza vizuri kwenye timu yao ya Polisi Tanzania.

Metacha na Makapu wameanza kwenye kikosi cha kwanza cha Polisi Tanzania katika michezo miwili ya ligi waliyocheza na yote wakiibuka na ushindi.


Katika michezo miwili waliyocheza Metacha ameruhusu bao moja tu, ambalo alifungwa na Azam juzi na timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.


Wakizungumza na Championi Jumatatu mastaa hao wamesema kuwa; “Nimefurahi kuanza kikosi cha kwanza nikiwa Polisi na mabeki wangu wapo vizuri naimani tutafanya vizuri msimu huu,” alisema Metacha.

“Mazingira na hata wachezaji wenzangu wapo vizuri na nahisi utakuwa mwaka mzuri sana kwangu,” alisema Makapu beki wa zamani wa Yanga.

CAREEN OSCAR, Dar es Salaam


 HABARI KAMA HIZI DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL KWA KUBONYEZA > HAPA

Post a Comment

0 Comments